KIBOKO YA AIR MANULA, LAKRED KWENYE HESABU ZA UNYAMANI

KIBOKO ya makipa wote wa Simba hivi karibuni kwenye mechi za ushindani ikiwa ni pamoja na kipa namba moja Aishi Manula, Ayoub Lakred na Ally Salim anatajwa kuwa kwenye hesabu za saini yake kuhitajika unyamani.

Ni Prince Dube mshambuliaji wa Azam FC raia wa Zimbabwe anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Simba ambao wanahitaji kuona anakuwa kwenye uzi wa rangi nyekundu.

Nyota huyo alikuwa anatajwa pia kuwa kwenye hesabu za Yanga lakini taarifa kutoka Azam FC hazijaitaja Yanga kuwa miongoni mwa timu ambazo zimepeleka ofa kuinasa saini ya nyota huyo.

Ikumbukwe kwamba Dube amewavuruga vibayavibaya Simba katika meçhi za ushindani jambo ambalo limewafanya watume ofa kuomba kuipata saini ya mwamba.

Sio Aishi Manula, Ally Salim, Ayoub Lakred wote wanalitambua balaa la Dube kwa kuwa amewatungua.

Mbali na Simba Klabu ya Al Hilal nayo imetajwa kwa timu ambazo zimetuma ofa kuipata saini ya Dube ambaye ameomba kuvunja mkataba na timu hiyo huku akitakiwa kulipa dola za Kimarekani laki tatu.