MBWANA SAMATTA AOMBA KUTOJUMUISHWA KWENYE KIKOSI KILICHOITWA KWA MICHEZO YA FIFA

Nahodha wa Timu ya Taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta ameomba kutojumuishwa kwenye kikosi kilichoitwa kwa michezo ya FIFA Series 2024.

Taarifa iliyotolewana Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), imeeleza kuwa Samatta amezungumza na kocha kabla ya kutajwa kwa kikosi hicho na kumuomba asijumuishwe katika safari ya Azerbaijan, ombi ambalo limekubaliwa.