AMEWEKA wazi kocha wa Geita Gold kwamba wanatambua ubora wa wapinzani wao ulipojambo linalowafanya waingie kwa tahadhari kwenye mchezo wa ligi.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Geita Gold ilipoteza pointi tatu muhimu kwa kufungwa maba 3-0 inatarajiwa kuwa kwenye mwendo wa kisasi kusaka ushindi uwanjani.
Denis Kitambi, Kocha Mkuu wa Geita Gold amebainisha kuwa wanatambua utakuwa ni mchezo mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wao lakini wanaimani watafanya vizuri.
“Tutaingia uwanjani kwa tahadhari ukizingatia kwamba hatupo kwenye nafasi nzuri kwa sasa hivyo ni muhimu kufanya maandalizi mazuri na kupata ushindi kwenye mchezo wetu,”.
Geita Gold mchezo wao uliopita ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji huku Yanga ikipata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Ihefu mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Yanga ina pointi 49 kwenye msimamo ni namba moja baada ya kucheza mechi 18 inakutana na Geita Gold yenye pointi 21 baada ya kucheza mechi 20.