KATIKA mechi tatu àmbazo ni dakika 270 Simba imeruhusu jumla ya mabao manne ikikwama kuondoka na clean sheet katika mechi hizo.
Ngoma ni nzito kwenye upande wa ulinzi huku benchi la ufundi likibainisha kuwa litafanyia kazi hayo yote kwenye uwanja wa mazoezi.
Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba amesema wanatambua kuwa kuna makosa yanatokea jambo wataalofanyia kazi uwanja wa mazoezi.
Safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao sita katika mechi hizo ilikuwa Simba 1-2 Tanzania Prisons, Coastal Union 1-2 Simba na kete ya kukamilisha dakika 270 ilikuwa Simba 3-1 Singida Fountain Gate.
Katika mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate walianza Simba kufunga dakika ya 6 na 9 kupitia kwa Saido Ntibanzokiza n Fredy Michael alipachika bao dakika ya 34.
Bao pekee la Singida Fountain Gate lilifungwa dakika ya 84 na Thomas Ulimwengu ikiwa ni bao lake la kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24.
Nafasi ya tatu Simba na pointi 42 baada ya kucheza mechi 18 huku safu ya ulinzi ikiwa imeruhusu mabao 18, Singida Fountain Gate nafasi ya 12 pointj 21.