UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa wale wanaosema ushindi wao kàtika mechi za Ligi Kuu Bara ni wa mchongo wajiulize wao walifungwa ngapi walipokutana nao.
Machi 11 2024 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 5-0 Ihefu na pointi tatu zikiwa ni mali ya Yanga.
Mabao ya Pacome Zouzoua dakika ya 10, Mudathir Yahya dakika ya 30, Aziz KI dakika ya 68, Okra Magic dakika ya 84 na Maxi Nzengeli dakika ya 85.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema:” Wale ambao wanasema ushindi wetu ni wa mchongo wajiulize wao tuliwafunga mabao mangapi kwa mchongo ama wao wamejificha?
Yanga ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 49, Azam FC nafasi ya pili pointi 44 namba tatu Simba pointi 39.
Ni kama dongo kimtindo kwa watani zao wa jadi Simba ambao nao walipokutana kwenye mchezo wa ligi Novemba 5 2023 walishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga.