KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Fountain Gate umebainisha kuwa unahitaji pointi tatu muhimu.
Ikumbukwe kwamba Simba imetoka kupata ushindi dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo wa ugenini uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu na pointi 39 baada ya kucheza mechi 17 vinara wa ligi ni Yanga wenye pointi 49 baada ya kucheza mechi 18.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya Singida Fountain Gate utakuwa na ushindani mkubwa lakini wanahitaji pointi tatu.
“Tunakwenda kwenye mchezo wetu dhidi ya Singida Fountain Gate tukiwa imara na tunahitaji pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo mashabiki wajitokeze kwa wingi,”.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 8:15 usiku kwa mujibu wa taarifa ya Simba ambayo ilitolewa ilikuwa inaeleza namna hii: “Uongozi wa Klabu ya Simba kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi umeona ni vyema mchezo wa dhidi Singida Fountain Gate kuanza saa 2:15 usiku ili kutoa nafasi ya kufuturu kwa mashabiki ambao watakuwa wamefunga,”.