RASMI leo Machi 12 2024 droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika imepangwa ambapo kila mmoja ametambua atakayekutana naye ndani ya uwanja kusaka ushindi kutinga hatua ya robo fainali.
Simba imepangwa kukutana na Al Ahly ya Misri wakati Yanga ikiangukia mikononi mwa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika michezo yao ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Wababe hawa wawili wanatambua kazi iliyopo mbele yao kusaka ushindi na wote wawili wataanzia nyumbani wakipoteza nyumbani kazi itakuwa ugenini kupindua meza kibabe.
Mechi za mkondo wa kwanza zitapigwa kati ya Machi 29-31 na kurudiana kati ya Aprili 5-7, 2024.
Ni ratiba kamili ya robo fainali na nusu fainali ipo namna hii:-
ROBO FAINALI
Simba dhidi ya Al Ahly
TP Mazembe dhidi ya Petro Atletico
Esperance dhidi ya ASEC Mimosas
Yanga dhidi ya Mamelodi Sundowns
NUSU FAINALI
Mshindi wa mchezo wa Esperance/ASEC dhidi ya mshindi wa Yanga/Mamelodi
Mshindi wa mchezo wa TP Mazembe/Petro Atletico vs Simba/Al Ahly.
Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania kwenye hatua hii ngumu yenye ushindani mkubwa.