LIGI YA MABINGWA ULAYA KUENDELEA LEO

Mtoto hatumwi dukani leo kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya ambapo itapigwa michezo ya kibabe katika hatua ya 16 bora ili kutoa tiketi ya robo fainali kwa vilabu vinne vitakavyocheza leo.

Leo itapigwa michezo miwili mikali ya ligi ya mabingwa ulaya ikihusisha timu nne ambapo michezo yote iko wazi na kila mmoja ana uwezo wa kufuzu hatua inayofuata, Arsena watakua nyumbani kuwakaribisha Fc Porto kutokana nchini Ureno wakati huo Barca nao watakua nyumbani kuwakaribisha klabu ya Napoli kutoka kule nchini Italia.

Arsenal wakiwa katika dimba la Emirates watakua na kazi moja tu kuhakikisha wanashinda mchezo huu ili kuweza kufuzu hatua ya robo fainali, Lakini wakati huohuo Fc Porto wana faida ya goli moja ambalo walilipata wiki mbili zilizopita katika dimba lao la nyumbani.

Arsenal ni wazi leo watahitahitaji kupata ushindi utakaoweza kuwapeleka mbele lakini klabu hiyo iliyo kwenye ubora mkubwa kwasasa watakua na mlima wa kupanda, Kwani Fc Porto ni klabu iliyoonekana kuzuia vizuri sana na kushambulia kwa kushtukiza. Mchezo huu utapatikana pale kwenye tovuti ya Meridianbet na umepewa ODDS KUBWA.

Mchezo mwingine mkali utapigwa pale katika dimba la Olympico Lluis kati ya klabu ya Barcelona dhidi ya Napoli ambapo Barca watakua nyumbani katika mchezo huo, Mchezo wa kwanza pale katika dimba la Diego Armando Maradona ulimalizika kwa sare ya goli moja kwa moja.

Mchezo huu utakua wazi kwa timu zote kwani yeyote atakaeshinda mchezo atakata tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali, Hivo mchezo huu unatarajiwa kua mkali na wenye ushindani mkubwa kwakua uko wazi na kila timu ina nafasi ya kusonga mbele.

Suka mkeka wako kwenye michezo mikali itakayopigwa leo kwenye ligi ya mabingwa Afrika, Machaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Bila kusahau ligi kuu ya NBC pia leo itaendelea ambapo Mnyama Simba atashuka dimbani kumenyana na klabu ya Singida Fountain Gate katika dimba la Chamazi jijini Dar-es-salaam, Ambapo Simba itahitaji kupata alama tatu muhimu ili kurejea kwenye mbio za ubingwa wa ligi hiyo.Mchezo huu mkali pia utapatikana pale kwenye tovuti ya Meridianbet ukiwa umepewa ODDS BOMBA kabisa