MSHAMBULIAJI KMC AINGIA ANGA ZA YANGA

NYOTA Wazir Junior mshambuliaji wa KMC ameingia anga za Yanga kwa kuwa sawa kwenye utupiaji na mwamba Aziz KI ndani ya Ligi Kuu Bara.

Ikumbukwe kwamba Junior aliwahi kucheza katika kikosi cha Yanga alipoibuka hapo akitokea Mbao lakini alikwama kuwa kwenye ubora kutokana na kutopewa nafasi mara kwa mara na hata alipopewa hakuwa na bahati yakufunga.

Wakati ubao wa Uwanja wa Azam Complex, Machi 10 2024 ukisoma KMC 4-2 Tabora United alitupia kambani mabao matatu na kusepa na mpira wake.

Ni dakika ya 49, 60, 67 alikamukisha hat trick na kufikisha mabao 11 sawa na Aziz Ki wa Yanga. Bao lingine ni mali ya Daruesh Saliboko.

Mabao ya Tabora United yalifungwa na Daniel Lukandamila dakika ya 84, 90 kwa mkwaju wa penalti.

KMC kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya nne na pointi 28 baada ya kucheza mechi 21, Tabora United ipo nafasi ya 14 pointi 21 baada ya kucheza mechi 21.