MWAMBA Willy Onana nyota wa Simba amefanya kitu ambacho kimeipa ushindi timu yake kwa kutimiza majukumu yake wakiibuka na ushindi ugenini dhidi ya CoastalUnion.
Baada ya dakika 90 ubao umesoma Coastal Union 1-2 Simba mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao umechezwa Uwànja wa Mkwakwani,Tanga.
Mabao ya Simba yamefungwa na Fred Michael dakika ya 11 na bao la ushindi limefungwa na Willy Onana dakika ya 73ambapo Onana alianzia benchi aliingia kipindi cha pili.
Bao la Coastal Union ni mali ya Lukas Kikoti dakika ya 24 ambaye alimchungulia namna Ayoub Lakred alipokuana kuachia shuti akiwa nje ya 18.
Mwamba wa LusakaClatous Chama amefanya kazi yake kwenye mchezo wa leo akitoa pasi mbili za mabao ndani ya dakika 90.
Ikumbukwe kwamba mchezo uliopita Simba ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons, imeibuka na pointi tatu ugenini.
Mchezo ujao Simba watarejea Azam Complex, Uwànja wa Jamhuri una tatizo kwenye upande wa Azam Media urushaji wa matangazo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania.