KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA COASTAL UNION, MANULA OUT

KUUMIA kwa Henock Inonga mwamba Che Malone anarejea kikosi cha kwanza dhidi ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union , Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mbali na Che Malone pia Aishi Manula kipa namba moja wa Simba hayupo kwenye mpango kazi wa leo ambapo benchi yupo Ally Salim.

Shomari Kapombe, Zimbwe, Kennedy Juma na Ayoub Lakred watakuwa kwenye ulinzi.

Babacar Sarr, Ntibanzokiza, Fabrince Ngoma, Fredy Michael, Chama na Miquissone wameanza kikosi cha Kwanza