Bingwa wa zamani wa uzito wa juu, Anthony Joshua amefanikiwa kumpiga kwa Knock Out (K.O) Francis Ngannou bingwa wa zamani wa UFC wa uzito wa juu katika pambano la Uzito wa Juu lililofanyika Riyadh, Saudi Arabia
Joshua alimwangusha Ngannou katika raundi ya kwanza ya mchezo na baadaye dakika ya 2:38 ya raundi ya pili alimwangusha tena kwa ngumi nzito ya mkono wa kulia, hatua iliyosababisha Mwamuzi kumaliza mchezo huo