MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa wanahitaji pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa, Machi 8 2024.
Yanga itamkosa Pacome, Djigui Diarra ambaye ni kipa namba moja kwenye mchezo wa leo kwa kuwa hawapo kwenye mpango wa kikosi hicho kilichopo Lindi.
Baaada ya kucheza mechi 16 Yanga ina pointi 43 ikiwa nafasi ya pili na vinara ni Azam FC wenye pointi 44 baada ya kucheza mechi 20.
Gamondi amesema wanatambua ushindani uliopo kwenye mechi za kitaifa na kimataifa hivyo jitihada itakuwa katika kubadilisha mbinu ili wachezaji wapata matokeo katika mechi hizo.
“Mchezo wetu dhidi ya Namungu utakuwa ni mzuri wenye ushindani kwa timu zote kwani hatujawahi kuwa na mchezo mwepesi dhidi ya Namungo..
“Tunahitaji pointi tatu kwenye mchezo wetu na tunaamini itakuwa hivyo, mashabiki wajitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu kuwa pamoja nasi,”.