SABABU YA SINGIDA FOUNTAIN GATE KUVUNJA BENCHI LA UFUNDI

UONGOZI wa Singida Fountain Gate umeweka wazi kuwa sababu kubwa ya kuvunja benchi lao la ufundi ni matokeo yasiyoridhisha kwenye mechi za hivi karibuni.

Machi 6 2024 uongozi wa Singida Fountain Gate ulibainisha kuwa umevunja benchi lake la ufundi lililokuwa chini ya Kocha Thabo Senong na msaidizi wake Nizar Khalfan.

Yote haya yanatokea kutokana na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha ambapo katika mechi tano za mwisho kwenye ligi kuu ya NBC, wameambulia sare moja pekee wakiwa wamepoteza kwenye mechi nne za ushindani.

Mara ya mwisho benchi hilo mbinu zake kutumika kwenye mchezo wa ligi walishuhudia wakipoteza kwa kufungwa mabao  2-0 na Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.