KOCHA SIMBA AMESEPA

KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha anatarajiwa kuondoka leo Machi 7 kwa ajili ya kuelekea nchini Algeria atakuwa huko kwa muda wa siku tano.

Machi 6 Benchikha alishuhudia kikosi cha Simba kikipigishwa kwata na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kocha huyo anakwenda Algeria kwa ajili ya kuchukua kozi na atarejea akishamaliza.

“Kocha Benchikha leo ataondoka nchini kwenda Algeria kwa ajili ya kushiriki kozi na atarejea nchini kuendelea na majukumu yake baada ya siku chache.

“Kwa wakati huu ambao atakuwa hayupo timu itakuwa chini ya kocha msaidizi Farid na Seleman Matola ambao wote wana uzoefu na atakosekana kwenye mechi mbili baada ya hapo atarejea kuendelea na majukumu yake,’.