AZAM FC WAPINDUA MEZA KIBABE

AZAM FC wamepindua meza kibabe baada ya kuambulia pointi moja mbele ya Coastal Union katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Baada ya dakika 90 ubao umesoma Azam FC 1-1 Coastal Union kwa wababe hao kugawana pointi mojamoja ambapo katika mzunguko wa kwanza Azam FC walivuna pointi tatu.

Bao la Coastal Union lilifungwa na Semfuko Charles dakika ya 68 na bao la Azam FC lilifungwa na Feisal Salum dakika ya 81.

Azam FC inafikisha jumla ya pointi 44 baada ya kucheza mechi 20 nafasi ya kwanza huku kinara wa utupiaji akiwa ni Feisal mwenye mabao 12.