KUNA kete za moto ndani ya kikosi cha Simba ambacho kina kazi nzito ya kusaka pointi tatu dhidi ya wapinzani wao ambao nao pia wanazihitaji pointi hizo tatu kwa namna yoyote ile kutoakana na ushindani wa ligi kuwa mkubwa.
Wakiwa wameshatinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika kazi inatarajiwa kuendelea ndani ya Ligi Kuu Bara wakiwa na kete nne za kukamilisha ambazo ni msako wa pointi 12 ndani ya dakika 540.
Simba iliyo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi 15 imekusanya pointi 36 inatarajiwa kuanza ikiwa nyumbani Uwanja wa Jamhuri, Morogoro Machi 6 dhidi ya Tanzania Prisons.
Kazi hiyo ikiisha kituo kinachofuata itakuwa Tanga dhidi ya Wagosi wa Kaya Coastal Union mchezo unatarajiwa kuchezwa Machi 9, Uwanja wa Mkwakwani.
Kete ya tatu itakuwa dhidi ya wakulima wa alizeti Singida Fountain Gate ngoma inatarajiwa kupigwa Machi 12 Morogoro, Uwanja wa Jamhuri.
Machi 15 2024 watakuwa Morogoro kumenyana na Mashujaa ya kutoka mwisho wa reli Kigoma ikumbukwe kwamba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na Saido Ntibanzokiza