MWAMBA FEI TOTO GARI LIMEWAKA HUKO

NYOTA Feisal Salum gari limewaka ndani ya uwanja kutokana na kasi yake kuzidi kupamba moto akiwa anatimiza majukumu yake ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani.

Mzawa huyo ni namba moja kwenye chati ya wafungaji Bongo akiwa katupia jumla ya mabao 11 yupo ndani ya Azam FC akitimiza majukumu yake na mechi za nyumbani huwa wanacheza Uwanja wa Azam Complex.

Mfungaji wa bao la kwanza ndani ya Azam FC ni yeye mwenyewe Fei Toto ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Tabora United alipofanya hivyo dakika ya tatu mapema kabisa kipindi cha kwanza.

Mbali na kuwa mfungaji wa bao la kwanza Azam FC pia ni mfungaji wa kwanza hat trick ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 ilikuwa kwenye mchezo huo wa kwanza wa mzunguko wa kwanza lakini walipokutana na Tabora United mzunguko wa pili ngoma ilikuwa 0-0.

Mabao mawili alifunga kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji Uwanja wa Azam Complex yalimfanya afikishe jumla ya mabao 11 akiwa ni haguo la kwanza kwa Yusuph Dabo kwenye upande wa viungo washambuliaji.

Azam FC ipo nafasi ya pili pointi 43 baada ya kucheza mechi 19 safu ya ushambuliaji imetupia mabao 44. Mchezo ujao kwa Azam FC ni dhidi ya Coastal Union unaoatarajiwa kuchezwa Machi 6 2024 Uwanja wa Azam Complex.