KITUO KINACHOFUATA SIMBA NI MOROGORO

BAADA ya kukamilisha mwendo katika hatua ya makundi na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kituo kinachofuata ni mchezo wa Ligi Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo wao wa mwisho katika hatua ya makundi msimu wa 2023/24 ilikuwa dhidi ya Jwaneng Galaxy hawakuwa na chaguo lolote zaidi ya kushinda.

Ushindi wa mabao 6-0 unawapa nafasi ya kuungana na timu 8 kwenye hatua ya robo fainali huku kutoka Tanzania zikiwa ni timu mbili pamoja na Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Mchezo ujao kwa Simba unatarajiwa kuchezwa Machi 6 Uwanja wa Jamhuri,Morogoro ambao ni wa Ligi Kuu Bara.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema wataingia uwanjani kwa tahadhari kutafuta pointi tatu.

“Ilikuwa ni kazi kubwa kwenye mechi za kimataifa na sasa tunarejea kuvaana na Tanzania Prisons itakuwa Morogoro hatujacheza muda mrefu pale hivyo burudani zinahamia Uwanja wa Jamhuri,”..