TIMU ZILIZOPO HATUA YA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

SHIRIKISHO la mpira barani Afrika limetangaza kuwa litapanga hivi karibuni siku maalumu kwaajili ya kupangwa kwa tarehe maalum ya kufanyika droo ya kupata timu ambazo zitafanikiwa kukutana kwenye robo fainali.

Tanzania imefanikiwa kuingiza timu mbili ambazo zimefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali.
Timu nyingine ni pamoja na Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, Esparence Tunis ya Tunisia, TP Mazembe ya DR Congo, Petro Luanda na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
Yanga ilianza kukamilisha safari kutoka kundi D kisha Simba ikafuata kwenye mchezo wake wa sita uliochezwa Uwanja wa Mkapa.