KIPA WA PENALTI AREJEA SIMBA

KIPA mwenye rekodi ya kuokoa penalti kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Ayoub Lakred hatua ya makundi ndani ya kikosi cha Simba amerejea kazini baada ya adhabu yake kukata hivyo kuna uwezekano wapinzani wao Jwaneng Galaxy wakakutana naye.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ugenini aliokoa penalti dakika ya 37 na kwenye mchezo huo walipoteza kwa kufungwa bao moja.

Alikosekana kwenye mchezo dhidi ya ASEC Mimosas ugenini Simba walipotoshana nguvu bila kufungana kwenye mchezo huo kutokana na adhabu ya kadi tatu za njano.

Langoni ni kipa namba moja wa Simba mzawa Aishi Manula alianza kikosi cha kwanza walipogawana pointi mojamoja hivyo kuna uwezekano mkubwa akawa sehemu ya kikosi kwenye mchezo ujao dhidi ya Jwaneng Galaxy unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 2.

Ikumbukwe kwamba Simba inatafuta nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali huku watani zao wa jadi Yanga wakiwa wamekamilisha hesabu mapema na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Al Ahly.

Njia pekee waliyobakiwa nayo Simba kuhakikisha wanatinga hatua hiyo ni kupata ushindi wa namna yoyote ile kwenye mchezo wao wa mwisho ambao watakuwa wapo nyumbani.