SIMBA WAPIGA HESABU HIZI KIMATAIFA

KUELEKEA mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopewa jina la Vita ya Kisasi huku mgeni rasmi akiwa ni beki Henoc Inonga benchi la ufundi limebainisha kuwa linahitaji ushindi.

Abdelahak Benchikha, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wanachohitaji kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy, Uwanja wa Mkapa ni ushindi.

Kikosi cha Simba kina kibarua cha kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wakipata ushindi wanakuwa na uhakika wa kutinga hatua ya robo fainali Afrika.

Ipo wazi kwamba watani wa jadi wa Simba ambao ni Yanga tayari wana uhakika wa kushiriki robo fainali wakiwa na pointi 8 baada ya kucheza mechi tano za makundi leo Machi Mosi watakuwa na kazi dhidi ya Al Ahly kukamilisha mchezo wa sita katika makundi.

Kocha wa Simba amebainisha kuwa wanahitaji matokeo kwenye mchezo wao bila kuangalia matokeo ya timu pinzani.

“Uzuri ni kwamba tutakuwa na mashabiki kwenye mchezo wetu na ambacho tunahitaji ni ushindi bila kujali matokeo ya timu nyingine muda ni sasa na tunaamini itakuwa hivyo kwa kuwa maandalizi yapo vizuri.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku Machi 2 2024.