SAMUEL ETO’O ATANGAZA K RIGOBERT SONG, MKATABA WAKE UMETAMATIKA RASMI

Rais wa Shirikisho la soka la Cameroon (Fecafoot), Samuel Eto’o ametangaza kuwa Rigobert Song, mkataba wake umetamatika rasmi.

Uvumi wa kufukuzwa kwa kocha huyo ulivuma tangu kuondolewa mapema kwa Cameroon, bingwa mara tano wa Afrika, mikononi mwa Nigeria katika hatua ya 16 bora ya AFCON 2023.

Rigobert Song ataondoka kwenye benchi la timu ya taifa, Rais wa Fécafoot, Samuel Eto’o ametangaza rasmi Jumatano Februari 28 katika mahojiano ya kipekee na FRANCE 24.