Skip to content
MIAMBA Azam FC wamezidi kujiongezea ngome nafasi ya pili baada ya kukomba pointi tatu mazima dhidi ya Singida Fountain Gate.
Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba ubao ulisoma Singida Fountain Gate 0-1 Azam FC bao lilifungwa na Kipre Junior dakika ya 53.
Azam FC inafikisha pointi 40 baada ya kucheza mechi 18 vinara ni Yanga wenye pointi 43 baada ya kucheza mechi 16.
Kipre Jr amesema kuwa ushindi huo kwake ni furaha hasa kwa kufunga bao lililowapa pointi tatu muhimu.
“Kwetu ni furaha kupata ushindi kwenye mchezo uliokuwa mgumu na tulikuwa tunahitaji pointi tatu ambazo tumezipata,’.