YANGA wameandika rekodi ya kutinga hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wapinzani wao CR Belouizdad mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Ushindi huo umewapa fursa Yanga chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi kuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya robo fainali kwa Tanzania huku Simba ikiwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa mwisho.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Mudathir Yahya dakika ya 43, Aziz KI dakika ya 47 Kenedy Musonda dakika ya 48 na Guede dakika ya 84.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (MwanaFA) amekabidhi kitita cha shilingi milioni 20 kwa Yanga SC baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad.
Fedha hizo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliahidi kutoa shilingi milioni tano kwa kila goli la ushindi kwenye michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.