SELEMAN Matola, kocha msaidizi wa Simba amesema mpango mkubwa kwa sasa ni kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy.
Ipo wazi kwamba mchezo uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundiilishuhudia ubao ukisoma ASEC Mimosas 0-0 Simba.
Ndani ya msako wa pointi tatu wababe hao wote wawili waligawana pointi mojamoja huku wakitambua kwamba tayari mtani wao wa jadi Yanga katinga hatua ya robo fainali.
Matola amesema kuwa kwenye mchezo dhidi ya ASEC Mimosas walikuwa wanahitaji pointi tatu iliposhindikana wakaamua kutafuta pointi moja.
“Kulikuwa na nafasi kwetu kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya ASEC Mimosas kutokana na nafasi ambazo tulitengeneza lakini ilishindikana kwa kuwa hatukuzitumia.
“Baada ya kukosa nafasi hizo ilitubidi tuttafute pointi moja sasa akili zetu ni mchezo wetu ujao dhidi ya Jwaneng Galaxy ambao tutakuwa nyumbani, mashabiki wajitokeze kwa wingi,”.
Kwenye mchezo uliopita ugenini miongoni mwa wachezaji walioanza kikosi cha kwanza ni Clatous Chama,Aishi Manula, Sadio Kanoute.
Mchezo ujao unatarajiwa kuchezwa Machi 2 2023 Uwanja wa Mkapa.