LIVERPOOL WAPINDUA MEZA NYUMBANI

WAKIWA Anflield wamebakiza pointi tatu mazima kwa USHINDI dhidi ya Luton Town mchezo wa Premier League.

Wababe hao walipindua meza kibabe wakiwa nyumbani na kukomba pointi tatu mazima.

Ni Chiedozie Ogbene alianza kufunga dakika ya 12 lilidumu mpaka wanakwenda mapumziko.

Dakika ya 56 beki Virgil van Dijk aliweka usawa, Cody Gakpo aliongeza bao la pili dakika ya 58, Luis Diaz dakika ya 71 na kamba ya nne ilipachikwa na Harvey Elliott dakika ya 90.

Mwisho ubao ulisoma Liverpool 4-1 Luton Town.

Liverpool nafasi ya kwanza na pointi 60 baada ya kucheza mechi 26 Manchester City nafasi ya pili pointi 56 baada ya kucheza mechi 25.

Luton Town ipo nafasi ya 18 na pointi 20 baada ya kucheza mechi 25.