ARAJIGA APATA SHAVU HUKO

KUTOKA Tanzania mwamuzi Ahmed Arajiga amepata shavu la kuwa miongoni mwa waamuzi kwenye mashindano ya All African Games ikiwa ni jambo la kujivunia hivyo ana kazi ya kuongeza umakini kwenye kutimiza majukumu yake.

Ipo wazi kuwa waamuzi wa Bongo wamekuwa wakiingia kwenye lawama mara kwa mara kutokana na kile kinachotajwa kutokuwa na maamuzi makini ya sheria 17 za mpira jambo linalowafanya wapewe adhabu pale wanapokwama kutafsiri sheria hizo.

Shirikisho la Soka Barani Afrika limemteua Ahmed Arajiga kuwa miongoni mwa waamuzi watakaochezesha Mashindano ya All African Games yatakayoanza  Machi 8, 2024 huko Ghana.

Tanzania ni mojawapo ya nchi zitakazoshiriki michuano hiyo na baadhi ya mataifa mengine kama Morocco, Senegal, Ghana, Algeria na Benin.