MWAMBA GUEDE NA OKRA WATAKATA MBELE YA POLISI TANZANIA

NYOTA wa Yanga, Joseph Guede na Okra Magic wametaka kwenye mchezo wa Azam Sports Federation dhidi ya Polisi Tanzania kwa kupiga kazi kubwa mwanzo mwisho.

Ni Februari 20 ubao wa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ulisoma Yanga 5-0 Polisi Tanzania ambao wanafungashiwa virago kwenye mashindano hayo .

Katika mchezo huo mabao yalifungwa na Guede ambaye amefungua pazia kwenye kutupia ndani ya Yanga alitupia mabao mawili dakika ya 13 na dakika ya 45 kwa pasi za Okra.

Farid Mussa alitupia bao moja dakika ya 33 na nyota Clement Mzize alifunga bao moja dakika ya 82 akiwa ndani ya 18.

Mzize alisababisha penalti dakika ya 85 ilifungwa na Shekhan Ibrahim ikiwa ni bao lake la kwanza ndani ya Yanga akiweka wazi kuwa ni furaha kwake kufanya hivyo.

“Nimefurahi kufunga na nilikuwa napenda kufanya hivyo jambo hili kukamilika ni furaha kwangu na nilipata nafasi ya kufunga haikuwezekana hivyo kwa kilichotokea ni furaha kwangu na timu kiujumla,”.