WAKIWA kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya CR Belouizdad Jumamosi, Uwanja wa Mkapa, Yanga leo wanakibarua mbele ya Polisi Tanzania.
Ni mchezo wa Azam Sports Federation hatua ya 16 bora unaotarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku sawa na muda wa mchezo wao ujao Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utachezwa Uwanja wa Mkapa.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kwamba wachezaji wapo tayari kuelekea kwenye mchezo huo na wanatambua kwamba ushindani ni mkubwa.
“Tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye mchezo wetu dhidi ya Polisi Tanzania, tunawaheshimu wapinzani wetu na tunaamini kwamba wachezaji wanajua umuhimu wa mchezo huu.
“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa kuwa uwepo wao unaongeza nguvu kwa wachezaji kufanya kazi kubwa kutafuta ushindi uwanjani,”.