KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas wawakilishi Simba wamebainisha kwamba maandalizi yapo tayari na mpango wao ni kupata matokeo mazuri.
Mchezo huo wa hatua ya makundi unatarajiwa kuchezwa Februari 23 siku ya Ijumaa kwenye msako wa pointi tatu kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wataanza safari mapema kuwafuata wapinzani wao ASEC Mimosas.
“Mchezo wetu dhidi ya ASEC Mimosas ni muhimu kwetu kupata pointi na kikosi Jumatatu kimefanya mazoezi ya mwisho hapa Dar na alfajiri Jumanne tunatarajia kuanza kuwafuata wapinzani wetu kwenye mchezo wetu muhimu.
“Kikubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu na inawezekana kutokana na maandalizi mazuri ambayo yanafanyika ni muda wetu kuwakilisha kwenye mechi za kimataifa na malengo ni kuendelea kufanya vizuri,”.