TATU BORA KIVUMBI, ZOTE ZASHINDA

LIGI Kuu Tanzania Bara ushindani wake unazidi kuwa mkubwa kila wakati huku tatu bora vita ikiwa ni kubwa Kwa kila timu.

Azam FC walifunga Februari 16 ubao ulisoma Azam FC 2-1 Geita Gold mabao yalifungwa na Tariq Seif dakika ya 41, Gibril Sillah dakika ya 44 na makali ya Idd Suleiman Nado yalionekana dakika ya 83 alipofunga bao la ushindi.

Azam FC inafikisha pointi 35 ikiwa nafasi ya pili, Simba nafasi ya pili pointi 36 vinara Yanga pointi 40 wote wamecheza mechi 15.

Timu zote zilizo ndani ya tatu bora kwenye mechi za kufunga mzunguko wa kwanza zimekomba pointi tatu mazima.

Tanzania Prisons 1-2 Yanga, JKT Tanzania 0-1 Simba na matajiri wa Dar walikamlilisha kete yao kwa ubao kusoma Azam FC 2-1 Geita Gold.