MCHEZAJI WA SPARTAK MOSCOW YA NCHINI URUSI, QUINCY PROMES, AKUMIWA KWENDA GEREZANI MIAKA 6

Mchezaji anayekipiga katika timu ya Spartak Moscow ya nchini Urusi, Quincy Promes, amehukumiwa kwenda Gerezani miaka 6 baada ya kukutwa na hatia ya uuzaji wa dawa za kulevya.

Promes ambaye aliwahi kuitumikia timu ya Taifa ya Uholanzi kati ya mwaka wa 2014-2021 hakuwepo wakati hukumu inatolewa katika mji wa Amsterdam Uholanzi.

Pia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye aliwahi kuzitumikia timu za Ajax Amsterdam na FC Seville, amehukumiwa kifungo cha miaka 18 kwa kumpiga na chuma kwenye magoti binamu yake mwaka wa 2020.

Quincy Promes anayekipiga Spartak Moscow tangu 2021 amesema anakewenda kukata rufaa.