>

HUYU HAPA MJASIRIAMALI AKOMBA MILIONI ZA SUPA JACPPOT YA SPORTPESA

KAMPUNI ya michezo na kubashiri Tanzania, SportPesa ambao ni wadhamini wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga wamemtangaza mshindi wa SportPesa Supa Jacpot ambaye ni kijana wa miaka 27.

Leo Februari 15 imefanyika hafla fupi ya kumpongeza kijana huyo David Mwenge Nyantora  ambaye ni mjasiriamali na kumkabidhi zawadi yake hiyo huku akiweka wazi kuwa ilikuwa ni furaha kubwa kwake kupata ushindi huo.

Ni mshindi wa SUPA JACKPOT 13/13 Millioni 265,780,681 ambazo kashinda baada ya kufanya utabiri makini kwenye Supa Jacpot alipochagua mechi 13.⁣

Amekomba mkwanja huo kwa kupatia mechi 13 kati ya 13 za SupaJackpot pia katika picha ni viwango vingine vya BONUS vya washindi wengine ⁣

Mshindi huyo amesema: “Nilifurahi sana baada ya kutangazwa kuwa mshindi lakini sikupata usingizi siku ambayo nilitangazwa kuwa mshindi kutokana na furaha ambayo ilikuwa ipo,”.