KIPA wa kazi ndani ya Yanga Djigui Diarra amerejea ndani ya kikosi hicho baada ya kuwa kwenye majukumu mengine ya timu ya taifa.
Tayari Diarra ambaye ni kipa namba moja wa Yanga yupo kambini na kikosi hicho baada ya kuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa lake la Mali iliyoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Vinara hao wa ligi wapo kwenye maandalizi ya mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya wakusanya mapato wa Dar KMC unaotarajiwa kuchezwa Februari 17,2024.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 5-0 KMC ukiwa ni ushindi mkubwa kupatikana mwanzo wa msimu.