>

KIJANA ASHINDA JACPOT YA BILIONI KUTOKA SPORTPESA

KAMPUNI ya Michezo na Burudani SportPesa imemtangaza mshindi wa Jackpot ya shilingi 265,780,681 TZS David Mwenge Nyantora (27).

David ambaye ni mwajiriwa alibashiri kwa usahihi mechi 13 kati ya 13 kwenye mechi za Supa Jackpot ambayo inamgawanyiko wa Jackpot za mechi 17,16,15,14 na 13 iliyopata mshindi.

Akimtangaza mshindi huyo wa awamu ya kumi Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa, Tarimba Abbas alianza kwa kumpongeza David kwa ushindi wake na kuwa milionea mpya mjini.

“Nifuraha yangu kubwa sana kwa niaba ya kampuni kumtangaza kwenu Davidi Mwenge Nyantora kuwa ni mshindi rasmi wa Supa Jackpot yetu ya mechi 13 akiwa amejishindia shilingi 265,780,681.

“Ikiwa ni takribani miezi 11 tangu kumtangaza mshindi wa mwisho wa Supa Jackpot mechi hizi hizi 13 na hii ikiwa ni awamu ya pili tangu kupata mshindi wa Supa Jackpot tangu ianzishwe rasmi.

“Hili ni jambo la kihistoria kwa kampuni ya kubashiri kupata zaidi ya washindi wa Jackpot 10 na kuwatangaza kwa miaka 6 mfululizo.

“Supa Jackpot ya wiki hii imeweza kutoa washindi wa bonasi jumla ya 8708 huku jumla ya bonasi zilizotolewa ikiwa ni zaidi ya milioni 756. Ni miaka saba sasa tangu kuanzishwa kwa kampuni ya SportPesa ikiwa imetangaza jumla ya washindi 10 wa Jackpot na maelfu ya washindi wa bonasi kila wiki,” amesema.