AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa itafahamika kuhusu suala la wao kudaiwa kwamba walikuwa wanamkimbia mpinzani wao Azam FC kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.
Leo Februari 9 2024 Simba inatarajiwa kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC, Uwanja wa CCM Kirumba ikiwa ni mchezo wa kiporo.
Mchezo uliopita kwa Simba ilipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tabora United mchezo uliochezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Ally amesema:”Walikuwa wanasema kwamba tumeikimbia mechi sijui kuna mengi juu yetu muda umefika na sasa itafahamika nani ambaye alikuwa anamkimbia mwenzake ndani ya uwanja.
“Tupo tayari kwa ajili ya mechi yetu dhidi ya Azam FC tunawaheshimu wapinzani wetu kikubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu,” amesema.
Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo dhidi ya Simba na wanahitaji pointi tatu.
“Tunatambua umuhimu wa mchez wetu dhidi ya Simba na tutaingia tukiwa hatuna uhakika wa kushinda,”.