YANGA NI KAZI JUU YA KAZI

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga ni kazi juu kazi ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na mechi zao kuwa bandika bandua.

Ikumbukwe kwamba Yanga chini ya Miguel Gamondi ambaye ni kocha mkuu ina kazi ya kutetea taji la ligi baada ya kutwaa 2022/23.

Inaendelea kupambania pointi tatu ndani ya ligi kwa Februari ilipofungulia kwa kuambulia sare Februari 2 2024 Uwanja wa Kaitaba.

Baada ya kuanzia Kagera dhidi ya Kagera Sugar ubao uliposoma Kagera Sugar 0-0 Yanga, Februari 4 ilikuwa ni Yanga 1-0 Dodoma Jiji na Februari 8 Yanga wanatarajiwa kuvaana na Mashujaa.

Ikumbukwe kwamba Mashujaa ya Kigoma ilitoka kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Simba, Uwanja wa Lake Tanganyika ubao uliposoma Mashujaa 0-1 Simba bao likifungwa na Saido Ntibanzokiza.

Yanga ni vinara wa Ligi Kuu Bara ni pointi 34 wamekusanya kibindoni baada ya kucheza mechi 13.