NYOTA SIMON MSUVA KAANZA KAZI NA TIMU YAKE MPYA

NYOTA  Simon Msuva hatimaye ameanza kazi kwenye timu yake mpya baada ya kuachana na timu yake ya zamani.

Ni Simon Msuva ambaye ni kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameanza rasmi mazoezi na timu yake ya mpya ya Al Najmah ya Saudi Arabia.

Kiungo huyo aliyekuwa anatajwa kurejea Yanga amesajiliwa kwenye timu yake hiyo mpya akitokea Klabu ya JS Kabylie.

Al Najmah katika Ligi Kuu Saudia imecheza mechi 19 na kuvuna pointi 25, ikishinda mechi 7, droo 4 na kupoteza mechi 8.

Ikumbukwe kwamba Msuva ni nyota pekee kutoka Taifa Stars ambaye alifunga bao kwenye AFCON 2023 Ivory Coast kwenye mchezo dhidi ya Zambia wa hatua ya makundi akitumia pasi ya nahodha Mbwana Samatta.