KIKOSI cha Simba kina kazi ya kukabiliana na Tabora United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwiny.
Simba imetoka kupata ushindi ugenini ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika uliposoma Mashujaa 0-1 Simba na bao likifungwa na Said Ntibanzokiza baada ya dakika 90.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa wanatambua ushindani uliopo na kikubwa ni kuona kwamba wanapata pointi tatu muhimu.
“Tunatarajia kucheza na Tabora United ni moja ya timu bora na ngumu, tunawaheshimu wapinzani wetu lakini ambacho tunahitaji ni kupata pointi tatu muhimu.
“Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kupambana na kupata ushindi,tunaamini kwamba tutawapa furaha Wanasimba, tuzidi kuwa pamoja,”.
Kibindoni Simba ina pointi 26 inakutana na Tabora United yenye pointi 15.