>

MZIZE AINGIA FAINALI KUWANIA TUZO

MSHAMBULIAJI wa Yanga , Clement Mzize ameingia kwenye orodha ya kumsaka mchezaji bora wa mwezi Januari.

Shindano Hilo linapewa nguvu na Shirika la Bima la NIC ikiwa ni lengo la kuongeza ushindani ndani ya Yanga.

Wengine ambao anapambana nao katika fainali ni beki Gift Fred na kiungo mshambuliaji Willsony Bogy.

Ikumbukwe kwamba Januari 30 Mzize alifunga mabao matatu kwenye ushindi wa mabao 5-0 dhidi yya Hausing FC ya Njombe kwenye mchezo wa raundi ya pili Azam Sports Federation.

Yanga ni mabingwa watetezi walicheza mchezo huo Uwanja wa Azam Complex.