>

MAJEMBE MAPYA SIMBA YAANZA NA 4G

IKIWA Uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa raundi ya pili Simba imeibuka na ushinsi wa mabao 4-0 Tembo FC.

Kila kipindi Simba ilifunga mabao mawili mawili katika mchezo ambao walitawala kwa kiasi kikubwa katika umiliki wa mpira huku umaliziaji ikiwa ni tatizo jingine.

Luis Miquissone alipachika bao dakika ya 11, Saidi Ntibanzokiza dakika ya 31, Saleh Karabaka dakika y 81 na Pa Jobe dakika ya 83.

Simba inaungana na Yanga katika hatua inayofuata ya Azam Sports Federation.

Majembe mapya ya Simba ambayo yamesajiliwa kwenye dirisha dogo yameanza kushuhudia  ushindi wa 4G ikiwa ni pamoja na Michael Fred, Pa Jobe, Balua ambao walipata nafasi ya kucheza kama ilivyokuwa kwa Karabaka na Ladack Chasambi.