MKALI wa mapigo huru ndani ya Ligi ya Wanawake Tanzania, Joele Bukuru aliyekuwa akicheza kikosi cha Simba Queens yupo tayari kwa kazi akiwa na timu yake mpya ya Singida Fountain Gate.
Ipo wazi kwamba kiungo huyo alipokuwa ndani ya kikosi cha Simba Queens alikuwa akipewa majukumu ya mapigo huru ikiwa ni faulo, kona kaanza mazoezi na timu yake mpya.
Changamoto mpya zinaanza ndani ya timu hiyo inayotarajiwa kuvaana na Simba Queens mabosi zake wa zamani waliotoka kupata ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Alliance Girls.
Mratibu wa Singida Fountain Gate, Issa Liponda, (Issa Mbuzi) ameliambia Championi Jumatatu kuwa maandalizi yanakwenda vizuri kwa ajili ya mechi zijazo.
“Maandalizi yapo vizuri na mchezo wetu ujao ni dhidi ya Simba Queens miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi ni pamoja na Bukulu, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” alisema Mbuzi.