>

SIMBA NA YANGA WAPINZANI WAO HAWA HAPA

AZAM Sports Federation Cup 2023/24 raundi ya pili inatarajiwa kupigwa ndani ya Januari baada ya ratiba kupangwa.

Tayari Simba na Yanga wameshawajua wapinzani wao kwenye hatua hiyo ambapo mechi zinachezwa kwa mtindo wa mtoano atakayepoteza mchezo safari inamkuta.

Kagera Sugar inayotumia Uwanja wa Kaitaba kwa mechi za nyumbani itamenyana na Dar City Januari 31 saa 10:00 jioni.

Mabingwa watetezi Yanga watavaana na Hausing FC Januari 30 Saa 1:00 usiku, Uwanja wa Azam Complex.

Mtibwa Sugar watamenyana na Nyakagwe FC, Januari 30 Uwanja wa Manungu Complex Saa 10:00 jioni.

Simba itacheza na Tembo FC Januari 31 ambapo muda na uwanja vitatajwa hivi karibuni.