IHEFU WAPO CHIMBO HUKO

WAKATI huu wa mapumziko ya Ligi Kuu Bara kutokana na kuwepo kwa mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika, maarufu kama AFCON uongozi wa Ihefu umeweka wazi kuwa kambi yao itakuwa Arusha mpaka pale ligi itakaporejea.

Kocha Mkuu wa Ihefu Mecky Mexime amesema kuwa uwepo wao ndani ya Arusha utawajega zaidi na watarejea wakiwa imara kwenye ligi kwa ajili ya kupambana kupata matokeo mazuri kwenye mechi za ushindani.

Mexime alikuwa anakifundisha kikosi cha Kagera Sugar alitambulishwa ndani ya Ihefu hivi karibuni kwa ajili ya kukifundisha kikosi hicho kinachotumia Uwanja wa Highland Estate kwa mechi za nyumbani.

Kocha huyo amesema: “Wachezaji wapo tayari kwa wale ambao wapo kwenye kikosi wapo wengine tunaamini watakuja kwa ajili ya kuendelea kufanya maandalizi ya mechi zetu zote za ushindani tupoa tayari na Arusha wametupokea vizuri.

“Uzuri ni kwamba hali ya hewa ya hapa sio tatizo ni nzuri kwetu wachezaji wanafurahia tunamuomba Mungu ligi itaaporejea tuwe kwenye mwendo mzuri kwa kuwa nafasi ambayo tupo kwa sasa sio nzuri kwetu,”