JANUARI 13 2024 mashindano ya Mapinduzi 2024 yaligota mwisho huku Mlandege wakitwaa taji hilo mara ya pili mfululizo kwa ushindi wa bao 1-0 Simba. Baada ya mchezo huo bosi wa Yanga ameweka wazi kuwa alitambua mapema kwamba hakuna timu iliyokuwa na uwezo wa kuizuia Mlandege kutwaa kwa mara ya pili taji hilo jambo ambalo limetimia.