ALI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa alitabiri tangu awali kuwa Mlandege walikuwa na nafasi ya kutwaa taji la Mapinduzi 2024 kwa mara nyingine tena.
Ipo wazi kuwa Januari 13,2024 ubao wa Uwanja wa New Amaan Complex ilikuwa Mlandege 1-0 Simba na taji likabaki Zanzibar.
Bao pekee la ushindi lilipachikwa dakika ya 54 na Joseph Akandwanao aliyewavuruga Simba kwenye mchezo huo kwa bao hilo lililodumu mpaka mwisho wa mchezo.
Kamwe baada ya Yanga kuondolewa hatua ya robo fainali na APR alisema: “Nimewaona Mlandege ni timu nzuri na wachezaji wanajituma hakuna timu inayoweza kuizuia kutwaa ubingwa hivyo nina amini itakuwa hivyo,”.