NGOMA AMKUNA BENCHIKHA SIMBA

KOCHA Mkuu wa Simba, Mualgeria Abdelhak Benchikha amefunguka kukoshwa na kiwango cha nyota wake, Fabrice Ngoma huku akisema kuwa amekuwa na msaada mkubwa kwa timu hiyo jambo ambalo kwake kama mwalimu anavutiwa nalo.

Ngoma ambaye amesajiliwa na Simba akitokea katika klabu ya Al Hilal ya Sudan, ni moja kati ya wachezaji wenye uhakika wa kucheza katika kikosi cha kwanza kutokana uwezo mkubwa anaouonyesha katika eneo la kiungo cha timu hiyo.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Benchikha alisema kuwa: “Ngoma ndio ni moja kati ya wachezaji ambao wameonekana kuwa na umuhimu katika kikosi changu lakini hilo sio kwangu pekee bali kote ambapo amepita Ngoma alikuwa anafanya vyema.

“Ni mchezaji ambaye huwa anapenda kuutawala mchezo lakini mara nyingi amekuwa akionyesha ile kiu ya kutaka kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri na inapata matokeo,hii imekuwa faida kwetu kwa Simba.

“Tunataka kuona timu kama Simba inakuwa na wachezaji wengi wenye uwezo na kuisadia timu kuzidi kuwa kubwa na yenye uwezo wa kuyapata mafanikio na hapo itakuwa ni faida zaidi kwetu katika mipango yetu ambayo tumejiwekea,” alisema Benchikha.