JANUARI 13 leo ni leo ambapo Michuano ya Mapinduzi Cup inafikia tamati kwa mechi ya fainali kupigwa
Mabingwa watetezi ambao ni Mlandege kucheza na Simba SC ambao wametinga hatua ya fainali 2024.
Ni bao la Fabrince Ngoma lilileta nongwa dakika za lala salama na kupelekea mikwaju ya penalti.
Singida Fountain Gate 2-3 Simba kwenye penalti baada ya kufungana bao 1-1 kwenye dakika 90 za jasho.
Mlandege wao walitinga hatua hii kwa ushindi mbele ya APR na Simba iliwaondoa Singida Fountain Gate.