HUYU HAPA CHAGUO LA KWANZA SIMBA

 KOCHA Mkuu wa Simba, Abdlehakh Benchika humwambii kitu kwa kiungo wa kazi Fabrince Ngoma ambaye hana jambo dogo kwenye majukumu yake ndani ya uwanja.

Ipo wazi kuwa Simba Jnuari 13 wanatarajia kucheza fainali dhidi ya Mlandege ambapo kwenye mechi zote tano ambazo walicheza tatu za makundi, moja robo fainali na moja hatua ya nusu fainali, mkata umeme Ngoma ilikuwa ni lazima aanze.

Sio kuanza tu, Ngoma alikuwa na uhakika wa kukomba dakika zote 90 hivyo kayeyusha dakika 450 kwenye mechi hizo akiwa ni chaguo la kwanza la Benchikha.

Ni Januari Mosi, JKU 1-3 Simba alianza kikosi cha kwanza alikomba dakika 90, Januari 3, Simba 2-0 Singida Fountain Gate, alianza kikosi cha kwanza alikomba dakika 90 na aliibuka mchezaji bora kwenye mchezo huo.

Januari 5, Simba 0-0 APR alianza kikosi cha kwanza na kukomba dakika zote 90, Januari 8, Simba 1-0  Jamhuri, alianza kikosi cha kwanza na alikomba dakika 90, Januari 10, hatua ya nusu fainali alianza kikosi cha kwanza na alikomba dakika 90 alifunga bao moja dakika ya 90+8.

Anatarajiwa kuanza pia kikosi cha kwanza leo dhidi ya Mlandege huku langoni Hussein Abel akitarajiwa kupewa kibarua cha kukaa langoni kwa kuwa Benchikha alikuwa akitoa mechi moja moja kwa kila mlinda mlango wake.